Taarifa kwa Vyombo vya Habari: Chaki Iliyovunjika (Broken Chalk) Inatoa Wito wa Kusitishwa Mara Moja kwa Mapigano ya Israeli na Jumuiya ya Kimataifa Kufuatia Mgogoro wa Hivi Punde katika Hospitali ya Al-Ahli Baptist

18 Ocktoba 2023

Tarehe ya 7 Oktoba, Hamas ilianzisha mashambulizi makubwa katika eneo la Israel wakati wa tamasha nje ya eneo jirani la ukanda wa Gaza. Tukio hili lilisababisha vifo vya zaidi ya raia 250 Waisraeli, huku wengine wengi wakitekwa nyara na kushikwa mateka katika eneo hilo. Kwa kujibu, Israel ilianzisha mzozo kamili dhidi ya Hamas, na kuanzisha mashambulizi ya anga huko Gaza na kuzingirwa kwa mpaka. Mzozo huu umekuwa na matokeo mabaya, huku takriban Wapalestina 3,000 wakipoteza maisha kutokana na shambulio la awali la Hamas, sambamba na kupoteza maisha ya zaidi ya raia 1,300 Waisraeli. Imesababisha mzozo mbaya wa kibinadamu kwa zaidi ya Wapalestina milioni 2 katika jiji lenye watu wengi zaidi ulimwenguni.

Tukitafakari juu ya gharama ya kibinadamu, inasikitisha kuona kwamba zaidi ya watoto 1,000 wamekufa huko Gaza tangu kuanza kwa vita, kama inavyokadiriwa na Wizara ya Afya ya Gaza. Kwa vile nusu ya wakazi milioni 2.3 wa Gaza wako chini ya umri wa miaka 18, Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa lazima ziongeze juhudi zao ili kuhimiza usitishaji mapigano mara moja na kuzichunguza pande zote mbili juu ya ufuasi wao wa sheria za kimataifa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano ya kibinadamu, akisema kuwa, “Mashambulio ya Hamas hayawezi kuhalalisha adhabu ya pamoja ya watu wa Palestina.”

Changamoto za mijadala inayoendelea hivi majuzi inayohusisha Marekani, Umoja wa Ulaya, Israel, na Misri zinatia wasiwasi sana. Lengo la msingi la mijadala hii ni kuwezesha kuingia kwa misaada muhimu ya kibinadamu kutoka Misri hadi Gaza kwa kufungua kivuko cha Rafah; cha kusikitisha ni kwamba, mazungumzo haya yamekabiliwa na vikwazo vikubwa, kwani Israel imelenga kivuko cha Rafah kwa mashambulizi ya angani mara nne tangu kuanza kwa mzozo tarehe 7 Oktoba. Mamia ya malori ya kibinadamu ya Misri yamekwama kwenye kivuko cha Rafah, huku serikali ya Misri ikiishinikiza Israel na Marekani kusimamisha mapigano ili misaada ya kibinadamu isiyo na kikomo ifikie wanaume, wanawake, na watoto wengi waliojeruhiwa.

Mnamo tarehe 17 Oktoba, mlipuko mkubwa uliitikisa Hospitali ya Al-Ahli Baptist huko Gaza, ambapo madaktari na wauguzi walikuwa wakiwahudumia Wapalestina waliojeruhiwa, wakiwemo wanawake na watoto, na Wapalestina wengine ambao walikuwa wakitafuta makazi. Tukio hili limekuwa eneo la idadi kubwa zaidi ya vifo vya tukio lolote tangu kuanza kwa mzozo wa sasa, na kusababisha vifo vya watu 500, kama ilivyoripotiwa na mamlaka ya afya ya Palestina. Wahusika wakuu wa kijeshi katika mzozo huo, Hamas na Jeshi la Ulinzi la Israeli, wanadai kuwa upande mwingine ulihusika na tukio hilo.

Wakati mzozo huu umeleta mgogoro wa kibinadamu ambao haujawahi kushuhudiwa, huku takriban Wapalestina milioni 2.2 wakiachwa bila kupata huduma za utangulizi kama vile chakula, maji, na umeme, Chaki Iliyovunjika(Broken Chalk) inapaza sauti yake kutaka hatua za haraka zichukuliwe kukomesha ukiukaji wa haki za binadamu unaoendelea ili kuleta madhara. Utulivu ndani ya kanda na kwa wanadamu wote. Tunatoa wito kwa serikali ya Israel na jumuiya ka kimataifa kufanya haraka ili kusitisha mapigano na kuruhusu misaada ya kibinadamu kupita kwenye mpaka wa Rafah, kuwapatia Wapalestina wengi waliokimbia makazi yao na walioathirika. Tunatoa wito kwa serikali ya Israel kutii kikamilifu sheria za kimataifa kuhusu kulinda hospitali, waandishi wa habari na raia. Tunaamaini ya kwamba ni muhimu kwamba jumuiya ya kimataifa ifanye uchunguzi zaidi kwa serikali ya Israel ili kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinazingatiwa. Ni dharura kwamba Israel iondoe mzingiro wa Gaza ili kuruhusu maji, chakula, umeme, na mafuta kufikia hospitali za Palestina.

Chaki Iliyovunjika (Broken Chalk) inatangaza kwa uma kwa heshima inayostahili.

Imetiwa sahihi na Chaki Iliyovunjika (Broken Chalk)

Chaki Iliyovunjika (Broken Chalk)

Translated by Lyndah Muthama from https://brokenchalk.org/press-release-broken-chalk-calls-on-the-immediate-ceasefire-by-israel-and-the-international-community-following-the-latest-crisis-at-al-ahli-baptist-hospital/

Hadithi ya Neslihan Ozcan Sahin: Baada ya mapambano yote, mwalimu mkimbizi anaanza kufundisha tena.

Imeandikwa na Georgette Schönberger

Neslihan ni mkimbizi kutoka Uturuki ambaye alikuja Uholanzi ili kujenga maisha mapya na mumewe na watoto wao wawili.

Mwezi Agosti 2018, Neslihan aliacha maisha yake Uturuki nyuma na kukimbia Ugiriki. Alikuwa huko kwa miezi mitatu kabla ya kuja Uholanzi. Amekuwa akiishi na familia yake katika nyumba za kijamii huko Amstelveen kwa miaka kadhaa. Aliishi na familia yake kwa muda wa miezi 19 katika vituo tofauti vya mapokezi ya wakimbizi (AZCs) nchini Uholanzi. “Ninajua Uholanzi vizuri zaidi kuliko Mholanzi wa kawaida,” anasema Neslihan.

Uturuki, Neslihan alikuwa amefanya kazi kama mwalimu wa kemia, fizikia, na biolojia kwa muda mrefu. Alikuwa na hamu ya kuanza kufundisha tena alipokuja Uholanzi. Bahati nzuri, kupata kazi haikuwa ngumu. Kupitia mradi wa “Statushouders voor de Klas”, alifundishwa jinsi mfumo wa shule ya Kiholanzi unavyofanya kazi, ambayo hatimaye ilimsaidia kupata mafunzo kazini. Aidha, Neslihan amefanya kazi kama mtoa huduma wa kujitolea katika shule. Huko alikuwa akifanya kazi kama msaidizi wa ufundishaji wa kiufundi katika shule ya upili ya Apollo huko Amsterdam. Katika shule hiyo hiyo, alikuwa na fursa ya kukua na baada ya muda, aliruhusiwa pia kufundisha siku mbili kwa wiki. Mwaka ujao atafundisha tu na hatafanya kazi tena kama msaidizi.

Kwa nini uliamua kuwa mwalimu wakati huo?

“Ninapenda kufundisha; Sioni hiyo kama kazi kwa sababu ni shauku yangu.” Amesoma kwa miaka 18 sasa na bado anafurahia sana. Baada ya kumaliza elimu yake, alianza kufundisha mara moja. Aliamua kuwa mwalimu wa kemia, fizikia, na biolojia kwa sababu alikuwa na alama za juu katika somo hizo tatu na aliziona kuwa mada za kufurahisha.

Kwa nini uliamua kuja Uholanzi?

“Tulisoma kwenye mtandao na habari na mara nyingi tulisikia kwamba Uholanzi, watu ni huru na wanaweza kushiriki maoni au mawazo yao. Kwa bahati mbaya, hii sio kesi nchini Uturuki, ambapo huwa huru na huwezi kusema unachotaka. Hata watoto mara nyingi wanakwenda gerezani kwa kufichua maoni yao”. Kwa sababu hii, ndugu na dada wa Neslihan pia walikuja Uholanzi na familia zao. Neslihan anawaona familia yake kila wiki.

Ulikabiliana na changamoto gani ulipofika Uholanzi?

Neslihan ni mkimbizi wa kisiasa na alikuwa akichukuliwa kama mtu wa kigaidi katika nchi yake kutokana na maoni yake. Pamoja na familia yake nzima, alilazimika kukimbia Uturuki kwa boti. Safari ya kufika Uholanzi ilikuwa ngumu. Alikuwa na kulipa fedha nyingi na kujadiliana na wasafirishaji wa watu, ambayo inaweza kuwa hatari sana.

Mbali na hayo, Neslihan alitaka kujifunza Kiholanzi; hii ilikuwa ngumu sana mwanzoni. Kwa sababu hakulazimika kujiunga wakati huo, hakuweza kuhudhuria kozi ya bure ya lugha ya Kiholanzi wakati wa kuishi kwake katika vituo vya mapokezi ya wakimbizi. Hata hivyo, aliweza kujifunza Kiholanzi kidogo kutoka kwa marafiki na wafanyakazi wa kujitolea katika vituo hivyo. Kwa hilo, anashukuru sana. Neslihan alitaka kujiunga na kufyonza tamaduni, kwa hivyo ufahamu wake wa lugha ulikuwa muhimu. Baada ya mapambano marefu, hatimaye alifanikiwa kukopa pesa ambazo alitumia kwa kozi.

Marafiki na wafanyakazi wa kujitolea katika AZC. Kwa hili, anashukuru sana. Neslihan alitaka kujiunga na kufyonza tamaduni, kwa hivyo ufahamu wake wa lugha ulikuwa muhimu. Baada ya mapambano marefu, hatimaye alifanikiwa kukopa pesa ambazo alitumia kwa kozi.

Kwa mara chache bado ana shida na lugha ya Kiholanzi, hasa ‘er’ na viambishi mbalimbali ambavyo anavipata vigumu. Aidha, bado haelewi baadhi ya mafumbo ya Kiholanzi, lakini anaamini kwamba hatimaye itatengemaa.

Je, kuna tofauti kati ya mfumo wa shule wa Uturuki na Uholanzi?

“Hakuna tofauti nyingi, nadhani. Bila shaka, mambo fulani ni sawa kabisa. Kwa mfano, vijana ni vijana tu na wanajitahidi kwa njia zinazofanana, lakini wanafunzi nchini Uholanzi wana fursa ya kuendelea kutokana na viwango tofauti vya shule. Kwa hivyo, mfumo wa Uholanzi ni bora kwa sababu fursa hiyo ipo.” Neslihan anaelezea kwamba nchini Uturuki, kuna kiwango kimoja tu na kila mwanafunzi lazima ajifunze masomo sawa na kufanya mtihani sawa. Kwa hiyo, ikiwa kiwango hiki ni kigumu sana, huna chaguo lingine la kuendelea kusoma, ndiyo maana vijana wengi wanakatisha masomo.

Tofauti nyingine kubwa ni kwamba kuna mamlaka kidogo nchini Uholanzi. “Mkurugenzi wangu na kiongozi wangu wa timu ni wenzangu tu. Tunachukuliwa kama sawa na kutendewa kwa njia ile ile. Nawaweza kuwaita kwa majina yao. Uturuki, lazima umwite kila mtu bwana au bibi. Sipendi kuwa na mamlaka zaidi nchini Uturuki; ningependa kubadilisha hilo”.

Je, kuna kitu chochote unachotaka kushiriki?

“Ningependa kusema kwamba sote ni binadamu ambao tunaweza kuishi pamoja; unapaswa tu kuwa na heshima kwa wengine. Lazima umtendee kila mtu kwa heshima na kuunda mazingira salama na mazuri. Tulikuja hapa kwa uhuru wetu, na Uholanzi imetupa haki nyingi. Kwa hiyo, lazima ufanye kitu kwa ajili ya Uholanzi; lazima utumie ujuzi wako kusaidia hapa, kujumuika. Kuchukua hatua ya kwanza ni rahisi: kusema “jambo” kwa majirani zako, kwa mfano, au tu kuzungumza na mtu na kuwa mwenye heshima.”

Neslihan pia alitaka kukumbusha kila mtu kwamba wengi bado wanatishiwa nchini Uturuki au wameachwa gerezani. Unaweza daima kufanya kitu kwa ajili yao, kwa mfano, kwa kushiriki kitu kwenye Twitter au kuzungumza juu yake.

Imetafsiriwa na Joseph Kamanga kutoka kwa asili https://brokenchalk.org/story-of-neslihan-ozcan-sahin-after-all-her-struggle-a-refugee-teacher-begins-to-teach-again/

Taarifa ya Habari: SIKU YA HAKI ZA BINADAMU 2022

 

10th December 2022

Taarifa ya Habari: SIKU YA HAKI ZA BINADAMU 2022

“Kurahisisha haki ya elimu kutawezesha kurahisisha haki zingine za binadamu”

Mnamo Desemba 10, Broken Chalk inapenda si tu kusherehekea miaka 74 ya Tamko la Pamoja la Haki za Binadamu, bali pia kuchunguza changamoto na mafanikio mengi ambayo jamii ya haki za binadamu imekabiliana nayo mwaka huu. Kama kawaida, lengo la Broken Chalk leo ni kueneza elimu kuhusu umuhimu wa elimu katika kutekeleza haki za binadamu. Licha ya maendeleo mengi katika haki za binadamu duniani kote, umaskini, ukatili wa kimfumo na taasisi, ubaguzi, na ufisadi bado unazuia watoto na vijana kutimiza haki yao ya elimu kikamilifu. Tunapoanza mwaka 2023, ni muhimu kuzingatia sera zipi nchi binafsi na jumuiya ya kimataifa zinapaswa kupitisha ili kuchochea elimu bora inayopatikana kwa wote.

Mwaka 2022, moja ya vikwazo kubwa vinavyozuia elimu hiyo kuendelea kuwa ufadhili. Vituo vya elimu ulimwenguni kote bado vinakosa miundombinu salama, maji safi, vifaa vya kutosha, vitabu, na vifaa vingine vya kufundishia. Walimu mara chache hulipwa mshahara wa kuishi licha ya kutekeleza kazi muhimu zaidi katika jamii. Mgogoro wa ufadhili huu unazidi kuwa mbaya kadiri bei za kimataifa zinavyoongezeka. Wakati uchumi unaporomoka, serikali zinapunguza bajeti ya elimu, ikipunguza zaidi ubora wa elimu inayotolewa. Wakati huo huo, familia zinahitaji kipato zaidi, hivyo watoto wengi wanakatisha masomo ili kufanya kazi. Mambo haya mawili yanajirudia; ikiwa ubora wa elimu anayopokea mtoto unapungua, familia zinazofanya tathmini ya gharama na faida zaidi zina uwezekano mkubwa wa kutoa kipaumbele kwa kazi kuliko shule kwa sababu kufanya kazi kunatoa thamani zaidi mara moja. Hii inaweza kuwa na athari kubwa; nguvu kazi isiyosoma inaweza kupunguza mishahara kwa wote, kuongeza pengo la kipato na kuongeza umaskini. Ili kuzuia mzunguko huu wa uovu, lazima tuwaambie watunga sera – kitaifa na kimataifa – kuwa elimu ni haki ya binadamu muhimu ambapo ufadhili wa kutosha unapaswa kutengwa.

Shida nyingine inayokabili elimu bora inayopatikana ni kuongezeka kwa migogoro ya ndani. Kutokana na mazoea ya ukandamizaji usiohaki unaotumiwa na serikali ya sasa nchini Uturuki, walimu wamekuwa wakifanyiwa mateso, kufungwa gerezani, na kupoteza maisha yao. Kati ya vurugu nchini Iran, mapinduzi ya mara kwa mara nchini Burkina Faso, uvamizi wa Ukraine, kuimarika kwa nguvu za Taliban nchini Afghanistan, na migogoro inayoendelea nchini Ethiopia, Syria, Yemen, Myanmar, na nchi nyingine nyingi, mwaka 2022 haukuleta mwisho wa migogoro mingi zaidi ulimwenguni. Katika maeneo yanayokabiliwa na migogoro, kutimiza haki ya binadamu ya elimu kunakabiliwa na changamoto kubwa. Tishio la mara kwa mara la vurugu linazuia elimu kutokea kabisa, hasa Kwa kuwa vituo vya elimu mara nyingi hulengwa na makundi yenye silaha. Familia zinapata hasara kubwa ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha, wanafamilia, mapato, na nyumba na hata kuwa wakimbizi au wakazi wa ndani. Kuimarisha juhudi za misaada ya kibinadamu ni muhimu ili kuhakikisha kuwa huduma za elimu za msingi zinaendelea kutolewa hata wakati wa migogoro. Elimu ni tiba nzuri ya kuzuia migogoro kabla haijatokea na kutibu athari za kijamii baada ya migogoro kutokea. Elimu ni muhimu katika kujenga mshikamano wa kijamii na inatoa njia isiyo ya vurugu ya kuelezea na kufikia malengo ya kisiasa. Katika jamii zenye hatari kubwa ya migogoro, elimu iliyolengwa inayosaidia makundi ya kijamii, kisiasa, na kikabila inaweza kuzuia vurugu. Ikiwa mgogoro utatokea ndani ya jamii, elimu baada ya tukio hilo inaweza kujaza pengo la maendeleo lililobaki na kuwasaidia kurejesha uchumi wa jamii. Elimu baada ya mgogoro pia inaweza kuwasaidia wale walioathiriwa hasi na mgogoro, hasa wale ambao wamepoteza maisha, familia au nyumba; elimu inaweza kutoa zana za uvumilivu na fursa mpya bora. Hatimaye, elimu ya haki za binadamu inaweza kurejesha wapiganaji wa zamani kwa kuwafundisha makosa ya tabia zao za vurugu na kuwafariji waathirika wa zamani kwa kuwafundisha kuthamini umuhimu wao kama binadamu.

Changamoto ya mwisho ambayo elimu inaendelea kukabiliana nayo ni dislokesheni inayosababishwa na janga la COVID-19. Wanafunzi wanaoathiriwa zaidi na kujifunza kidijiti, ikiwa ni pamoja na watoto wadogo na wale ambao hawawezi kumudu mtandao au teknolojia ya kidijiti, wanaendelea kudidimia katika shule. Lazima tuweze kuzuia kile kinachoitwa “mgogoro wa kimataifa wa kujifunza,” kwani watoto hawapokei ubora wa elimu uliokuwepo kabla ya COVID-19 na shule zinashindwa kubadilika kwa mahitaji yanayobadilika ya karne ya 21. Wapolicymakers wa kitaifa na kimataifa lazima watafute maoni kutoka kwa shule na familia ili kujifunza jinsi sera za elimu zinaweza kubadilika katika enzi ya kidijiti na jinsi ukidigitali unaweza kuwajumuisha wanafunzi wa asili mbalimbali na mahitaji ya kujifunza.

Katika mwaka 2023, Broken Chalk itajikita katika masuala haya pamoja na mengine. Ni muhimu kukumbuka Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu hii kwamba haki zote za binadamu zinaunganishwa na kuzalishana; kuwezesha haki ya elimu kutahamasisha haki nyingine za binadamu, kama haki za maisha, usawa mbele ya sheria, faragha, mali, uhuru wa mawazo, dhamiri na dini, uhuru wa maoni na kujieleza, na zingine nyingi. Kwa upande wa kurudiproku, maendeleo katika haki nyingine za binadamu yataathiri kwa njia chanya elimu.

Broken Chalk inatoa ahadi kwamba katika Mwaka Mpya huu, tutafanya kazi kwa bidii kuendeleza haki zote za binadamu kwa kukuza haki ya elimu.

Imesainiwa na

Broken Chalk

Human Rights Day 2022 Press Release_Eng

Mahojiano na Melek Kaymaz

Imeandikwa na Georgette Schönberger

Kutafsiriwa na Joseph Kamanga

Melek Kaymaz ni mkimbizi kutoka Uturuki na kwa sasa anafanya kazi kama mwalimu wa hesabu katika shule ya kimataifa ya upili huko Amsterdam. Shuleni anafundisha hesabu kwa Kihaolandi kwa wanafunzi wa Mavo, Havo, na Vwo.

 

Ulifika Uholanzi vipi?

Melek alikimbia Uturuki na mumewe. Kabla ya kuja Uholanzi, walikuwa wanaishi Iraq kwa miaka mitatu, ambapo Melek alifanya kazi kama mwalimu wa hesabu. Walipogundua kwamba Melek alikuwa mjamzito, walijua kwamba kurudi Uturuki na kubaki Iraq sio chaguo tena. Walitaka kufanya kitu kwa ajili ya binti yao, kwa mustakabali bora. Awali, hawakuwa na wazo la kwenda wapi, kama alivyoeleza Melek, “Hatukuwa na visa ya kwenda nchi ya Ulaya, wala ‘kadi ya kijani’ ya kwenda Marekani.” Baada ya kutumia muda kuchunguza fursa zao kwenye mtandao, waligundua kwamba Uholanzi ni nchi ambapo wakimbizi wanakaribishwa, wanaweza kupata msaada na wako huru. “Uhuru, huo ni muhimu sana kwangu, ndiyo sababu tulikuja Uholanzi”. Sasa Melek na mumewe wamekuwa wanaishi Uholanzi kwa miaka mitano.

“Hatua hii ilikuwa kubwa sana, na, mwanzoni, nilikuwa na wakati mgumu sana kuzoea, sikujua maana ya kuishi Uholanzi. Sikujua lugha bado na sikuwa na ujuzi wowote kuhusu utamaduni wa Kiholanzi.” Yeye na mumewe walikuja Uholanzi peke yao, kwani hawana jamaa au marafiki wanaoishi Uholanzi.

 

Kwa nini ukawa mwalimu wa hesabu?

“Wakati nilipokuwa mdogo, sio ndoto yangu kuwa mwalimu wa hesabu. Baadaye katika maisha nililazimika kufanya uchaguzi, kwa upande gani nilitaka kwenda. Nilijua ninalipenda hesabu. Nayaona hesabu kama mchezo au puzzle ambao ninataka kushinda. Zaidi ya hayo, nilijua pia kwamba ninapenda kufundisha hesabu kwa watu wengine. Mara nyingi nililazimika kufafanua mambo kwa ndugu zangu au familia yangu na nilifurahi sana kufanya hivyo. Kwa hiyo, uamuzi wa kuwa mwalimu wa hesabu ulikuwa uamuzi mzuri sana.”

 

Je, changamoto gani umekutana nazo?

Wakati Melek na mumewe walipofika Uholanzi, walilazimika kuanza upya. Hawakujua lugha au utamaduni wa Kiholanzi. Katika kituo cha mapokezi ya wakimbizi (AZC) huko Amsterdam, Melek alijifunza misingi ya lugha ya Kiholanzi kwa kutumia kitabu alichopata hapo. Alimaliza kuishi kwa miezi 10 katika kituo cha AZC pamoja na mumewe na binti yao aliyezaliwa hivi karibuni. Sasa anaishi katika nyumba pamoja na familia yake kusini-mashariki mwa Amsterdam. Ili kuboresha Kiholanzi chake, alisoma kozi ya bure iliyotolewa na manispaa ya Amsterdam. Pia alimaliza “Oriëntatietraject Statushouders voor de Klas” katika Hogeschool van Amsterdam. Kozi hii ilimsaidia sio tu kutawala lugha ya Kiholanzi, bali pia kumfundisha mfumo wa elimu ya Kiholanzi na kumwezesha kupata mafunzo ya vitendo kwenye shule ya upili.

 

Sasa bado anafanya kazi katika shule hiyo hiyo kama mwalimu wa hesabu. Mchakato huu unaonekana rahisi kuliko ilivyokuwa. Melek alitueleza kwamba alipata ugumu sana kupata kazi ya kufundisha. Kwa mfano, alituma maombi zaidi ya shule 40 ambazo ni chache sana ndizo zilizojibu. Mwishowe, alikuwa na chaguo kati ya shule mbili. Alikuwa na huzuni kubwa kuwa baadhi ya shule hazikujibu kabisa. “Mimi ni tofauti, nafahamu hilo, lakini nina matarajio ya kupata majibu, haswa kwa sababu Uholanzi ina uhaba wa walimu.”

Melek alihisi kwamba watu wa Kiholanzi hawakumwamini kwanza. “Wanaogopa watu wengine, hawaamini kwanza, lakini mara unapopata imani yao, basi ni mzuri na wana uchangamfu.”

 

Je, kuna tofauti gani kati ya mfumo wa elimu wa Kituruki na Kiholanzi?

“Elimu ya Kiholanzi kidogo inatofautiana na ile ya Kituruki.” Kwa mfano, Melek alitueleza kwamba shule nchini Uturuki pia zina ngazi tofauti. Lakini tofauti ni umri ambao watoto wanabadilisha ngazi. Kwa mfano, shule ya msingi nchini Uturuki pia ina miaka nane, lakini watoto nchini Uholanzi huanza shule ya upili wakiwa na umri mdogo zaidi. Kwa sababu hii, Melek alihisi kwamba idadi ya watoto wa Kiholanzi ambao wanaanza shule ya upili ni kidogo. Melek aligundua kwamba watoto wa Kiholanzi ni huru zaidi. “Watoto hapa ni wachangamfu zaidi. Uturuki, mwalimu lazima awe 100% mchanganuzi na wanafunzi wanafuata tu kile kinachosemwa. “Huko Uholanzi, watoto hufanya kazi bila msaidizi wa mwalimu kuelezea kila kitu.” Tofauti nyingine ni kwamba huko Uholanzi kuna shule nyingi tofauti, kama vile shule za umma, za kibinafsi, au za Kikristo. Nchini Uturuki, kuna aina moja tu ya shule.

 

Mtazamo wa siku za usoni

Licha ya kwamba Melek anamkosa familia na marafiki wake nchini Uturuki na utamaduni wake, bado anafurahi na uamuzi wake wa kuja Uholanzi. Familia yake na marafiki wana bahati ya kumtembelea mara kwa mara lakini yeye mwenyewe hawezi kwenda Uturuki. Kitu muhimu kwake ni uhuru anaoupata Uholanzi. Melek anapenda kuwasiliana na wakimbizi wengine kwamba mwanzoni ni hatua ngumu sana kuja Uholanzi na kuwa mwalimu hapa, lakini kamwe usikate tamaa na daima fanya bidii yako. Inazidi kuwa rahisi na rahisi na wakati.

 

Translated by Joseph Kamanga from https://brokenchalk.org/interview-with-melek-kaymaz/

.