Imeandikwa na Georgette Schönberger
Kutafsiriwa na Joseph Kamanga
Melek Kaymaz ni mkimbizi kutoka Uturuki na kwa sasa anafanya kazi kama mwalimu wa hesabu katika shule ya kimataifa ya upili huko Amsterdam. Shuleni anafundisha hesabu kwa Kihaolandi kwa wanafunzi wa Mavo, Havo, na Vwo.
Ulifika Uholanzi vipi?
Melek alikimbia Uturuki na mumewe. Kabla ya kuja Uholanzi, walikuwa wanaishi Iraq kwa miaka mitatu, ambapo Melek alifanya kazi kama mwalimu wa hesabu. Walipogundua kwamba Melek alikuwa mjamzito, walijua kwamba kurudi Uturuki na kubaki Iraq sio chaguo tena. Walitaka kufanya kitu kwa ajili ya binti yao, kwa mustakabali bora. Awali, hawakuwa na wazo la kwenda wapi, kama alivyoeleza Melek, “Hatukuwa na visa ya kwenda nchi ya Ulaya, wala ‘kadi ya kijani’ ya kwenda Marekani.” Baada ya kutumia muda kuchunguza fursa zao kwenye mtandao, waligundua kwamba Uholanzi ni nchi ambapo wakimbizi wanakaribishwa, wanaweza kupata msaada na wako huru. “Uhuru, huo ni muhimu sana kwangu, ndiyo sababu tulikuja Uholanzi”. Sasa Melek na mumewe wamekuwa wanaishi Uholanzi kwa miaka mitano.
“Hatua hii ilikuwa kubwa sana, na, mwanzoni, nilikuwa na wakati mgumu sana kuzoea, sikujua maana ya kuishi Uholanzi. Sikujua lugha bado na sikuwa na ujuzi wowote kuhusu utamaduni wa Kiholanzi.” Yeye na mumewe walikuja Uholanzi peke yao, kwani hawana jamaa au marafiki wanaoishi Uholanzi.
Kwa nini ukawa mwalimu wa hesabu?
“Wakati nilipokuwa mdogo, sio ndoto yangu kuwa mwalimu wa hesabu. Baadaye katika maisha nililazimika kufanya uchaguzi, kwa upande gani nilitaka kwenda. Nilijua ninalipenda hesabu. Nayaona hesabu kama mchezo au puzzle ambao ninataka kushinda. Zaidi ya hayo, nilijua pia kwamba ninapenda kufundisha hesabu kwa watu wengine. Mara nyingi nililazimika kufafanua mambo kwa ndugu zangu au familia yangu na nilifurahi sana kufanya hivyo. Kwa hiyo, uamuzi wa kuwa mwalimu wa hesabu ulikuwa uamuzi mzuri sana.”
Je, changamoto gani umekutana nazo?
Wakati Melek na mumewe walipofika Uholanzi, walilazimika kuanza upya. Hawakujua lugha au utamaduni wa Kiholanzi. Katika kituo cha mapokezi ya wakimbizi (AZC) huko Amsterdam, Melek alijifunza misingi ya lugha ya Kiholanzi kwa kutumia kitabu alichopata hapo. Alimaliza kuishi kwa miezi 10 katika kituo cha AZC pamoja na mumewe na binti yao aliyezaliwa hivi karibuni. Sasa anaishi katika nyumba pamoja na familia yake kusini-mashariki mwa Amsterdam. Ili kuboresha Kiholanzi chake, alisoma kozi ya bure iliyotolewa na manispaa ya Amsterdam. Pia alimaliza “Oriëntatietraject Statushouders voor de Klas” katika Hogeschool van Amsterdam. Kozi hii ilimsaidia sio tu kutawala lugha ya Kiholanzi, bali pia kumfundisha mfumo wa elimu ya Kiholanzi na kumwezesha kupata mafunzo ya vitendo kwenye shule ya upili.
Sasa bado anafanya kazi katika shule hiyo hiyo kama mwalimu wa hesabu. Mchakato huu unaonekana rahisi kuliko ilivyokuwa. Melek alitueleza kwamba alipata ugumu sana kupata kazi ya kufundisha. Kwa mfano, alituma maombi zaidi ya shule 40 ambazo ni chache sana ndizo zilizojibu. Mwishowe, alikuwa na chaguo kati ya shule mbili. Alikuwa na huzuni kubwa kuwa baadhi ya shule hazikujibu kabisa. “Mimi ni tofauti, nafahamu hilo, lakini nina matarajio ya kupata majibu, haswa kwa sababu Uholanzi ina uhaba wa walimu.”
Melek alihisi kwamba watu wa Kiholanzi hawakumwamini kwanza. “Wanaogopa watu wengine, hawaamini kwanza, lakini mara unapopata imani yao, basi ni mzuri na wana uchangamfu.”
Je, kuna tofauti gani kati ya mfumo wa elimu wa Kituruki na Kiholanzi?
“Elimu ya Kiholanzi kidogo inatofautiana na ile ya Kituruki.” Kwa mfano, Melek alitueleza kwamba shule nchini Uturuki pia zina ngazi tofauti. Lakini tofauti ni umri ambao watoto wanabadilisha ngazi. Kwa mfano, shule ya msingi nchini Uturuki pia ina miaka nane, lakini watoto nchini Uholanzi huanza shule ya upili wakiwa na umri mdogo zaidi. Kwa sababu hii, Melek alihisi kwamba idadi ya watoto wa Kiholanzi ambao wanaanza shule ya upili ni kidogo. Melek aligundua kwamba watoto wa Kiholanzi ni huru zaidi. “Watoto hapa ni wachangamfu zaidi. Uturuki, mwalimu lazima awe 100% mchanganuzi na wanafunzi wanafuata tu kile kinachosemwa. “Huko Uholanzi, watoto hufanya kazi bila msaidizi wa mwalimu kuelezea kila kitu.” Tofauti nyingine ni kwamba huko Uholanzi kuna shule nyingi tofauti, kama vile shule za umma, za kibinafsi, au za Kikristo. Nchini Uturuki, kuna aina moja tu ya shule.
Mtazamo wa siku za usoni
Licha ya kwamba Melek anamkosa familia na marafiki wake nchini Uturuki na utamaduni wake, bado anafurahi na uamuzi wake wa kuja Uholanzi. Familia yake na marafiki wana bahati ya kumtembelea mara kwa mara lakini yeye mwenyewe hawezi kwenda Uturuki. Kitu muhimu kwake ni uhuru anaoupata Uholanzi. Melek anapenda kuwasiliana na wakimbizi wengine kwamba mwanzoni ni hatua ngumu sana kuja Uholanzi na kuwa mwalimu hapa, lakini kamwe usikate tamaa na daima fanya bidii yako. Inazidi kuwa rahisi na rahisi na wakati.
Translated by Joseph Kamanga from https://brokenchalk.org/interview-with-melek-kaymaz/
.
No comment yet, add your voice below!