Taarifa kwa Vyombo vya Habari: Chaki Iliyovunjika (Broken Chalk) Inatoa Wito wa Kusitishwa Mara Moja kwa Mapigano ya Israeli na Jumuiya ya Kimataifa Kufuatia Mgogoro wa Hivi Punde katika Hospitali ya Al-Ahli Baptist

18 Ocktoba 2023

Tarehe ya 7 Oktoba, Hamas ilianzisha mashambulizi makubwa katika eneo la Israel wakati wa tamasha nje ya eneo jirani la ukanda wa Gaza. Tukio hili lilisababisha vifo vya zaidi ya raia 250 Waisraeli, huku wengine wengi wakitekwa nyara na kushikwa mateka katika eneo hilo. Kwa kujibu, Israel ilianzisha mzozo kamili dhidi ya Hamas, na kuanzisha mashambulizi ya anga huko Gaza na kuzingirwa kwa mpaka. Mzozo huu umekuwa na matokeo mabaya, huku takriban Wapalestina 3,000 wakipoteza maisha kutokana na shambulio la awali la Hamas, sambamba na kupoteza maisha ya zaidi ya raia 1,300 Waisraeli. Imesababisha mzozo mbaya wa kibinadamu kwa zaidi ya Wapalestina milioni 2 katika jiji lenye watu wengi zaidi ulimwenguni.

Tukitafakari juu ya gharama ya kibinadamu, inasikitisha kuona kwamba zaidi ya watoto 1,000 wamekufa huko Gaza tangu kuanza kwa vita, kama inavyokadiriwa na Wizara ya Afya ya Gaza. Kwa vile nusu ya wakazi milioni 2.3 wa Gaza wako chini ya umri wa miaka 18, Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa lazima ziongeze juhudi zao ili kuhimiza usitishaji mapigano mara moja na kuzichunguza pande zote mbili juu ya ufuasi wao wa sheria za kimataifa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano ya kibinadamu, akisema kuwa, “Mashambulio ya Hamas hayawezi kuhalalisha adhabu ya pamoja ya watu wa Palestina.”

Changamoto za mijadala inayoendelea hivi majuzi inayohusisha Marekani, Umoja wa Ulaya, Israel, na Misri zinatia wasiwasi sana. Lengo la msingi la mijadala hii ni kuwezesha kuingia kwa misaada muhimu ya kibinadamu kutoka Misri hadi Gaza kwa kufungua kivuko cha Rafah; cha kusikitisha ni kwamba, mazungumzo haya yamekabiliwa na vikwazo vikubwa, kwani Israel imelenga kivuko cha Rafah kwa mashambulizi ya angani mara nne tangu kuanza kwa mzozo tarehe 7 Oktoba. Mamia ya malori ya kibinadamu ya Misri yamekwama kwenye kivuko cha Rafah, huku serikali ya Misri ikiishinikiza Israel na Marekani kusimamisha mapigano ili misaada ya kibinadamu isiyo na kikomo ifikie wanaume, wanawake, na watoto wengi waliojeruhiwa.

Mnamo tarehe 17 Oktoba, mlipuko mkubwa uliitikisa Hospitali ya Al-Ahli Baptist huko Gaza, ambapo madaktari na wauguzi walikuwa wakiwahudumia Wapalestina waliojeruhiwa, wakiwemo wanawake na watoto, na Wapalestina wengine ambao walikuwa wakitafuta makazi. Tukio hili limekuwa eneo la idadi kubwa zaidi ya vifo vya tukio lolote tangu kuanza kwa mzozo wa sasa, na kusababisha vifo vya watu 500, kama ilivyoripotiwa na mamlaka ya afya ya Palestina. Wahusika wakuu wa kijeshi katika mzozo huo, Hamas na Jeshi la Ulinzi la Israeli, wanadai kuwa upande mwingine ulihusika na tukio hilo.

Wakati mzozo huu umeleta mgogoro wa kibinadamu ambao haujawahi kushuhudiwa, huku takriban Wapalestina milioni 2.2 wakiachwa bila kupata huduma za utangulizi kama vile chakula, maji, na umeme, Chaki Iliyovunjika(Broken Chalk) inapaza sauti yake kutaka hatua za haraka zichukuliwe kukomesha ukiukaji wa haki za binadamu unaoendelea ili kuleta madhara. Utulivu ndani ya kanda na kwa wanadamu wote. Tunatoa wito kwa serikali ya Israel na jumuiya ka kimataifa kufanya haraka ili kusitisha mapigano na kuruhusu misaada ya kibinadamu kupita kwenye mpaka wa Rafah, kuwapatia Wapalestina wengi waliokimbia makazi yao na walioathirika. Tunatoa wito kwa serikali ya Israel kutii kikamilifu sheria za kimataifa kuhusu kulinda hospitali, waandishi wa habari na raia. Tunaamaini ya kwamba ni muhimu kwamba jumuiya ya kimataifa ifanye uchunguzi zaidi kwa serikali ya Israel ili kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinazingatiwa. Ni dharura kwamba Israel iondoe mzingiro wa Gaza ili kuruhusu maji, chakula, umeme, na mafuta kufikia hospitali za Palestina.

Chaki Iliyovunjika (Broken Chalk) inatangaza kwa uma kwa heshima inayostahili.

Imetiwa sahihi na Chaki Iliyovunjika (Broken Chalk)

Chaki Iliyovunjika (Broken Chalk)

Translated by Lyndah Muthama from https://brokenchalk.org/press-release-broken-chalk-calls-on-the-immediate-ceasefire-by-israel-and-the-international-community-following-the-latest-crisis-at-al-ahli-baptist-hospital/

No comment yet, add your voice below!


Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *